Tanzania Bara inatarajiwa kucheza na timu za
Ethiopia, Zambia na Somalia katika mashindano ya Chalenji maarufu kama CECAFA
Challenge Cup yatakayofanyika nchini Ethiopia baadae mwezi huu.
Tanzania Bara itacheza na timu hizo kufuatia
kupangwa kundi moja na timu hizo ambapo mashindano yenyewe huenda yakafanyika
kati ya Novemba 21 na Desemba 6 mwaka huu.
Kwa mujibu wa tovuti ya Kawowo Sports ya nchini
Uganda, makundi hayo yametokana na droo iliyochezeshwa leo huko mjini Addis
Ababa nchini Ethiopia.
Kenya ndiyo bingwa mtetezi baada ya kushinda taji
hilo mwaka 2013 kwenye fainali zilizopigwa mjini Nairobi.
Ikumbukwe kwamba mashindano hayo hayakuweza
kufanyika mwaka jana baada ya nchi zilizotarajiwa kuwa mwenyeji kupigiana
danadana ikiwemo Ethiopia.
MAKUNDI
YA CECAFA 2015
Group A: Ethiopia, Zambia, Tanzania, Somalia
Group B: Kenya, Uganda, Burundi, Djibouti
Group C: Sudan, Rwanda, South Sudan, Zanzibar
No comments:
Post a Comment