Kocha Mkuu wa Taifa Stars Salum Shaban Mayanga ameiwezesha Stars kufika hatua ya nusu Fainali ya michuano ya COSAFA inayoendela Afrika Kusini.
Kocha huyo ambae
amekua akikosolewa sana wa wadau wa mpira
pamoja na mashabiki wa soka
Tanzania mara baada ya kutoka sare ya goli 1 kwa 1dhidi ya Lesotho katika
mchezo wa kufania kufuzu mataifa huru ya Afrika, lakini jana amewaumbua
mashabiki hao ambao wamekua wakimbza.
Zifuatazo ni rekodi ambazo Mayanga
amezivunja.
KOCHA Salum Mayanga ameweza kuiendesha Stars kwa mechi 7 bila
kupoteza tangu awe kocha mkuu ameshinda 4 na sare 3 na kuvunja rekodi ya Maximo.
Maximo aliweza kuiendesha stars kupata matokeo katika
michezo 5 na katika mitano hiyo alishinda 2 na kutoka sare 3 na mchezo wake wa 6 aliangukia pua kwa
kipigo cha 4-0 kutoka kwa Senegal ya kina Mamadou Niang.
MAYANGA Rekodi zake:
Tanzania v Botswana =2-0
Tanzania v Burundi =2-1
Tanzania v Lesotho =1-1
Tanzania v Malawi =2-0
Tanzania v Angola =0-0
Tanzania v Mauritius 1-1
Afrika Kusini v Tanzania 0-1
MARCIO MAXIMO :
Tanzania v Burkinafaso = 2-1
Tanzania v Kenya =0-0
Tanzania v Angola 1-1
Tanzania v Msumbiji =0-0
Tanzania v JK Congo
=2-0
Tanzania v Senegal 0-4
Hizo ni Takwimu za Mayanga vs Maximo za michezo yao ya
kwanza
Makocha waliomfuata Marcio Maximo ambao ni Jan Poulsen
(Denmark),Kim Poulsen (Denmark) ,Mart Nooij (Netherlands) na Boniphace Mkwasa (Tanzania) hakuna aliyefikia rekodi
hizi za kocha Mayanga.
No comments:
Post a Comment