MKURUGENZI wa zamani wa klabu
ya Real Madrid Jorge Valdano anaamini kuwa Raul anaweza kurejea Santiago
Bernabeu kama kocha mkuu katika siku zijazo na kujitengenezea jina kama ilivyo
kwa Pep Guardiola.
Raul aliondoka Madrid na kuhamia Schalke mwaka 2010 kabla ya
kuondoka katika timu hiyo ya Ujerumani na kwenda Al Sadd miaka miwili baadae
lakini Valdano hana shaka kwamba mshambuliaji huyo mkongwe mwenye umri wa miaka
36 anaweza kurejea kuingoza klabu hiyo kwa mafanikio kama iliyokuwa alipokuwa
mchezaji.
Valdano amesema hana shaka kwamba hivi Raul anajipima kama anaweza
kurejea Madrid akiwa kocha kwani anaweza kuongeza kitu muhimu kwa timu hiyo.
Guardiola ambaye amewahi kucheza Barcelona alirejea tena katika timu hiyo akiwa
kocha kati ya mwaka 2008 na 2012 akishinda mataji 14 kabla ya kuamua kupumzika
kwa muda wa mwaka mmoja na kurejea kuinoa Bayern Munich.
No comments:
Post a Comment