Beki wa pembeni Mbelgiji, Marnick Vermijl mwenye umri wa miaka 22, amechezea mara kadhaa kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 21 cha timu yake ya taifa na kwa sasa yupo kwa mkopo NEC Nijmegen msimu huu.
Akizungumza na Hets Nieuwsblad, wakala wa Vermijl aitwaye Tony Dullers amesema: “Yupo ndani ya mkataba na Manchester United hadi Juni 2015, lakini zaidi itategemea na mazingira ya David Moyes.
+6
+6
Zao la uzalishaji vijana: Mbelgiji huyo alitua Manchester United akitokea Standard Liege mwaka 2010
“Ikiwa kocha atabaki, kisha haitaonekana vizuri, kwa sababu alimuacha Marnick aende kwa urahisi NEC. Ikiwa Moyes atafukuzwa, inaweza kufungua nafasi kubwa (ndani ya United).
“Kwa Manchester United, wanafurahia sana maendeleo yake. Wanataka Marnick afanye kazi katika klabu bora msimu ujao, lakini si kutolewa kwa mkopo tena. Aidha anaweza kupata nafasi katika kikosi cha kwanza, au kuuzwa moja kwa moja,”.
Dullers amesema kwamba Ajax na klabu nyingine kadhaa za Ligi Kuu Engand zimeonyesha nia ya kumsajili beki huyo, wakati atakutana pia na Genk na Anderlecht wiki zijazo.
No comments:
Post a Comment