Wednesday, 26 February 2014

AZAM KUKIPIGA HII LEO DHIDI YA ASHANT UNITED DIMBA CHAMAZI



AZAM FC leo itashuka kwenye uwanja wake wa nyumbani kucheza mchezo wa kiporo kati yake na Ashanti United
Mechi itazikutanisha timu za Azam FC inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 37 dhidiya Ashanti United iliyoko nafasi ya 12 kwa pointi zake 14.

Ashanti United ndiyo timu pekee iliyofanikiwa kupata sare chamazi katika raundi ya kwanza na leo itajaribu kurejearekodi yake kwa angalau kuizuia Azam FC kama ilivyofanya Tanzania Prisons wikiendi iliyopita
Kikosi cha Azam FC leo kitawakosa baadhi ya nyota wake kutokana na kuwa na kadi au kuwa majeruhi
Wachezaji ambao watakosekana leo ni Salum Abubakar (Majeruhi) John Bocco na Kipre Tchetche (kadi)
Azam FC huenda ikawatumia baadhi ya chipukizi wake toka kwenye academy ili kuziba pengo hilo

Kikosi cha Azam FC kinachoanza leo ni
1. Mwadini Ally
2. Erasto Nyoni
3. Gardiel Michael
4. Said Moradi
5. Aggrey Morris
6. Kipre Bolou
7. Himid Mao
8. Brison Raphael
9. Gaudence Mwaikimba
10. Brian Omony
11. Khamis Mcha
Subs
Aishi Salum
David Mwantika
Ibrahim Mwaipopo
Mudathir Yahya
Kone Ismael
Abdallah Seif Karihe
Kevin Friday

No comments:

Post a Comment