MSHAMBULIAJI nyota wa zamani wa kimataifa wa
Brazil, Ronaldo de Lima amedai kuwa hana shaka kuwa Gareth Bale na
Cristiano Ronaldo watatengeneza muungano mzuri katika klabu ya Real
Madrid. Bale mwenye umri wa miaka 24 alitua Santiago Bernabeu kwa
uhamisho uliovunja rekodi wa euro milioni 100 katika kipindi cha usajili
wa majira ya kiangazi na kuzidi kiwango ambacho Madrid walimnunua
Ronaldo kutoka Manchester United mwaka 2009. Hata hivyo, nguli huyo wa
soka wa Brazil hadhani kama kuwasili kwa mchezaji mwingine mwenye jina
kwenye klabu hiyo kutamuathiri Ronaldo na kudai kuwa watacheza vyema
wakiwa pamoja. Ronaldo amesema wawili hao watawapa furaha mashabiki wa
Madrid kutokana na umahiri wao wa kucheza na kutengeneza nafasi za
kufunga. Bale anatarajiwa kucheza mechi ya kwanza akiwa na Madrid
mwishoni mwa wiki hii dhidi ya Villarreal.
No comments:
Post a Comment