KIPA
Joe Hart anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya tayari kwa kujiunga na klabu ya West Ham United kwa mkopo kutoka
Manchester City
West
Ham walikuwa wakitafuta kipa mpya kipindi hiki cha majira ya kiangazi na
wamefanikiwa kumshawishi kipa huyo wa kimataifa wa Uingereza.
Mkataba
wa Hart unatarajiwa kumalizika mwaka 2019 katika klabu ya City na inadaiwa kuwa
tayari alishaambiwa atafute klabu mpya na meneja Pep Guardiola.
City
walimruhusu Hart aende kwa mkopo katika klabu ya Torino msimu uliopita na sasa
anatarajiwa kuhamia Uwanja wa London huku Guardiola akiwa tayari kumlipa nusu
ya mshahara wake.
No comments:
Post a Comment