Uchaguzi wa Chama cha Mpira wa Miguu kwa Wanawake (TWFA), sasa utafanyika Dar es Salaam badala ya Dodoma na Morogoro - mikoa iliyotangazwa awali.
Mwenyekiti Kamati ya Uchaguzi ya TWFA,
Msomi Wakili George Mushumba, amesema kwamba taratibu zote zimekamilika na
kwamba siku ya uchaguzi ni Jumamosi Julai 8, mwaka huu.
Wakili Mushumba ametoa wito kwa wajumbe
wote kufika Dar es Salaam Ijumaa Julai 7, mwaka huu kwa ajili ya kufahamu
tararibu za awali za uchaguzi.
Tayari Kamati ya Mushumba ilitangaza
majina ya wagombea 11 waliopitishwa kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi
mkuu.
Majina ambayo yamepitishwa ni Amina
Karuma, Rose Kisiwa, Somoe Ng’itu, Theresia Mung’ong’o, Hilda Masanche, Salma
Wajeso, Zena Chande, Triphonia Temba, Mwamvita Kiyogoma, Jasmine Soudy na
Chichi Mwidege.
Nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti,
Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa
Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji.
No comments:
Post a Comment