Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya
Chama cha Wataalamu wa Tiba za Michezo (TASMA), kimetangaza Uchaguzi Mkuu wa
chama hicho kwamba utafanyika Agosti 5, mwaka huu katika Ukumbi wa Manispaa ya
Kinondoni, Dar es Salaam.
“Wanachama wote wanakaribishwa kushiriki
kwa namna moja au nyingine katika zoezi hili muhimu sana,” amesema Mwenyekiti
wa kamati hiyo, Leslie Liunda alipokuwa anatangaza ramani ya mchakato wa
uchaguzi huo leo Alhamis Julai 06, 2017.
Amesema: Mwanachama ye yote anayependa
kukiongoza chama hiki anaombwa kuchukua fomu katika ofisi za Olimpiki Maalumu,
zilizoko jirani na Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam kwa ajili ya kugombea nafasi
anayoona kuwa anaweza kuimudu.”
Nafasi zinazowaniwa ni Mwenyekiti,
Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina ambao fomu zao
zinapatikana kwa Sh 200,000 wakati nafasi za wajumbe wa Mkutano Mkuu TFF na
Wajumbe wa Kamati ya Utendaji fomu zao zinapatikana kwa Sh 100,000.
No comments:
Post a Comment