Friday, 7 July 2017

TETESI ZA USAJILI IJUMAA YA LEO.



Mustakabali wa meneja wa Chelsea, Antonio Conte uko mashakani baada ya meneja huyo kukasirishwa na shughuli nzima ya usajili katika klabu hiyo (Daily Mirror).



Hatua ya Manchester United kutaka kumsajili Romelu Lukaku, 24, haihusiani na mkataba ambao utamrejesha Wayne Rooney, 31, Everton (Liverpool Echo).

Chelsea bado wanatarajiwa kujaribu kumsajili Romelu Lukaku, 24, licha ya taarifa kuwa mchezaji huyo amekubali kuhamia Manchester United kwa pauni milioni 75 kutoka Everton (Guardian).

Mshambuliaji wa Real Madrid Alvaro Morata, 24, ameachwa "kwenye mataa" baada ya Manchester United kumsajili Romelu Lukaku. Morata alikuwa na uhakika kuwa anahamia Old Trafford (Independent).

Romelu Lukaku amekubali kusaini mkataba wa muda mrefu Manchester United na mshahara wa pauni 250,000 kwa wiki (Daily Star).

Chelsea huenda wakakabiliwa na tatizo la mshambuliaji baada ya Diego Costa kuanza kuaga wachezaji wenzake kufuatia kuambiwa na Antonio Conte kuwa hayuko kwenye mipango yake msimu ujao (Daily Telegraph).

Chelsea wanajiandaa kutoa dau "kubwa" kumtaka kiungo wa Real Madrid James Rodriguez (AS).

Chelsea sasa wameelekeza macho yao kwa mshambuliaji wa Swansea Fernando Llorente, 32, baada ya kushindwa kumpata kwa mkopo mwezi Januari (Evening Standard).

Haki miliki ya picha Getty Images Image caption Carles Puyol
Barcelona wamekasirishwa na nahodha wao wa zamani Carles Puyol, baada ya mchezaji anayemwakilisha Eric Garcia, 16, kuamua kuhamia Manchester City (Independent).

No comments:

Post a Comment