MSHAMBULIAJI
wa Atletico Madrid, Fernando Torres amesaini mkataba wa mwaka mmoja ambao
utamuweka katika klabu hiyo mpaka Juni mwaka 2018.
Mara
baada ya kusaini kandarsi hiyo mpya, Torres amesema amefurahishwa kuendelea
kubakia hapo kwa mwaka mmoja zaidi.
Baada
ya kuibuka katika kikosi cha kwanza cha Atletico mwaka 2001, mshambuliaji huyo
aliimarika na kuwa nahodha kabla ya kujiunga na Liverpool mwaka 2007.
Torres
ambaye ametwaa mataji mwili ya Ulaya na moja la Kombe la Dunia akiwa na
Hispania, pia amecheza kwa vipindi vifupi Chelsea na AC Milan kabla ya kurejea
Atletico mwaka 2015.

No comments:
Post a Comment