Aliekua
mchezaji wa klabu ya soka ya simba Ibrahimu Ajibu amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia
klabu ya soka ya Yanga.
Ajibu ambae
ameichezea Simba michezo 24 katika ligi kuu na kufunga magoli 8 amejiunga ma
mabingwa watetezi wa ligi hiyo kuongeza nguvu ya kupachika mabao.
Katika
kipindi akiwa Simba kwa msimu uliomalizika Ajibu amecheza dakika 1, 365 kwa
michezo 24 aliyoichezea simba huku michezo 17 akianza na kufanyiwa mabadiloko
kwa michezo 7 na michezo miwili akisotea kwenye benchi.
Ajibu sasa
anaungana na wachezaji wenzake kwenye safu ya ushambuliaji wa Yanga kama Saimon
Msuva, Obrey Chirwa, Amis Tambwe na Donald Ngoma.
No comments:
Post a Comment