Friday, 28 July 2017
TETESI ZA USAJILI IJUMAA YA LEO.
Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane amesema hawezi kutoa hakikisho kuwa Gareth Bale atabakia Bernabeu msimu huu, huku Manchester United wakimfuatilia. (Mirror)
Monaco watakuwa tayari kumuuza Kylian Mbappe kwa timu itakayokuwa tayari kutoa euro milioni 180. (L'Equipe)
Meneja wa Chelsea Antonio Conte anapanga kutoa pauni milioni 50 kuwasajili Ross Barkley, 23, kutoka Everton na Alex Oxlade-Chamberlain, 23, kutoka Arsenal. (Sun)
Chelsea wamepanda dau kutaka kumsajili kwa mkopo Renato Sanches, 19, kutoka Bayern Munich. (Daily Telegraph)
Meneja wa Tottenham Mauricio Pochetitino anataka kumsajili Ross Barkley na kumfanya kuwa kiungo wa kati. (Times)
Roma wanajiandaa kupanda dau jipya la pauni milioni 32 kumtaka winga wa kimataifa wa Algeria, Riyad Mahrez, anayechezea Leicester. (Mirror)
Liverpool wapo tayari kutoa dau la mwisho la zaidi ya pauni milioni 70 kujaribu kumsajili kiungo wa RB Leipzig Naby Keita, 22. (Mirror)
Liverpool wanashikilia msimamo wao kuwa Philippe Coutinho, 25, hauzwi, huku Barcelona wakiendelea kumfuatilia. (ESPN)
Limerpool- kwa shingo upande- wameweka bei ya Philippe Coutinho kuwa ni pauni milioni 133, kama kweli Barcelona wanamtaka mchezaji huyo kutoka Brazil. (Sport)
Meneja wa Inter Milan Luciano Spalletti amesema anataka Ivan Perisic kubakia Italia, ingawa hana uhakika kama ataweza kufanya hivyo huku Manchester United wakiendelea kumfuatilia. (ESPN)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment