Klabu
ya Simba kwa masikitiko makubwa inakanusha taarifa potofu zinazosambaa
mitandaoni na kwenye baadhi ya vyombo vya habari,kuwa imecheza mechi ya
kirafiki nchini Afrika kusini,na kupoteza mchezo huo.
Uzushi
huo unasema Simba imefungwa mchezo huo kwa jumla ya goli 7-0, na timu ya daraja
la kwanza ya nchini humo, Royal Eagles.
Kiukweli
Simba haina rekodi za hovyo kama hizo kokote inapocheza duniani,na haijawahi
kufungwa na klabu yoyote idadi ya magoli kama hayo,kama zilivyo klabu nyingine
nchini,hususan klabu ambayo mashabiki wake ndio wanaozusha upuuzi huo.
Dunia
ya leo ni ya Teknolojia, na ingekuwa ni kweli,hakuna mtanzania ambae asingeiona
hii taarifa kutoka kwenye mitandao au vyombo vya habari vya Afrika
kusini.
Tunapenda
Umma wa watanzania utambue kwa siku zote tulizokuwa huko,program ya benchi la
ufundi, ilijikita ktk kuitengeneza miili ya wachezaji kistamina.
Wiki
ijayo Timu yetu inatarajiwa kucheza mechi mbili na klabu za Orlando Pirates na
Bidverst za nchini humo, kabla ya kurejea tarehe tano mwezi ujao teyari kwa
mchezo wetu wa *SIMBA DAY* utakaopigwa tarehe nane mwezi ujao.
*Mwisho*
tunawaomba
wanachama na mashabiki wetu puuzeni uzushi wa mitandaoni, na taarifa rasmi
zitatolewa kwa mujibu wa taratibu rasmi za klabu.
No comments:
Post a Comment