Kikosi
cha Taifa Star leo kitashuka dimbani kutupa karata yake ya mwisho kusaka
mshindi wa tatu wa kombe la COSAFA dhidi ya Lesotho.
Kocha
mkuu wa kikosi hicho Salim Mayanga amefanya mabaliko kwenye kikosi hicho
kuelekea kwenye mchezo huo ambao utatoa taswira ya nani awe mshindi wa tatu
katika michuano hiyo.
Katika
mchezo wale Mayanga amemwanzisha golini Saidi Mohamed namba mbili ni Shomari Kapombe
huku namba tatu akicheza Gadiel Michael, nne na tao wanacheza Salim Mbonde na
Nurudin Chona,
Himid
Mao yeye atacheza namba sita namba nane ikichezwa na Salmin Hoza kumi ikichzwa
na Raphael Daudi, mambinga ni Shiza Kichuya na Simon Msuva, mpachika mabao
atacheza Stamil Mbonde.
Kikosi
cha leo Mayanga amepanga wachezaji wote wanaocheza ligi ya nyumbani kwa lengo
la kujipanga kwaajili ya mchezoo wa CHANI dhidi ya Rwanda Siku ya Jumamosi
ijayo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.
No comments:
Post a Comment