Katika
kikosi chake kabla ya kuivaa Rwanda Jumamosi ijayo, wachezaji wengine ambao
Kocha Mayanga amewatangaza leo ni pamoja na Kipa wa Serengeti Boys - timu ya
taifa a vijana ya Tanzania, Ramadhan Kabwili.
Mbali
ya hao wamo pia Boniface Maganga kutoka Mbao FC, Joseph Mahundi kutoka Azam FC
na pia amemrejesha tena Said Ndemla wa Simba SC ambaye awali alikuwa kwenye
uangalizi wa majeraha.
Kikosi
hicho kinakwenda kujiandaa na mchezo dhidi ya Rwanda utakaofanyika Uwanja wa
CCM Kirumba, Mwanza Jumamosi ya Julai 15, mwaka huu
Kipa
Benno Kakolanya, Shaban Idd Chilunda na Mbaraka Yussuf hao wamepumzishwa kwa
sababu ya majeraha waliyoyapata kwa nyakati tofauti wakiwa na Taifa Stars huko
Afrika Kusini kwenye michuano ya Kombe la Castle la Cosafa - inayoandaliwa na
Baraza la Soka kwa nchi za Kusini mwa Afrika.
Pia
wachezaji wa kimataifa ambao hawahusiki na mechi za CHAN ambao ni Thomas
Ulimwengu na Elius Maguri, hawakuongozana na timu.
Timu
hiyo ilishika nafasi ya tatu katika michuano ya Castle Cosafa kwa kuishinda
Lesotho kwa mapigo 4-2 ya penalti katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Moruleng
nchini Afrika Kusini Ijumaa iliyopita.
Mwanza
inajiandaa na mchezo dhidi ya Rwanda unaotarajiwa kufanyika Jumamosi Julai 15,
mwaka huu kuwania kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa
wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN).
Timu
hiyo ambayo kwa mwaka huu imecheza mechi tisa za kimataifa na kushinda mitano;
kutoka sare miwili na kufungwa mmoja wa nusu fainali za Cosafa, itakuwa na
kikosi cha wachezaji 24.
No comments:
Post a Comment