MSHAMBULIAJI
mpya wa Everton, Wayne Rooney amesema anasubiri kwa hamu ziara ya Tanzania
akiwa na klabu hiyo.
Rooney
aliyerejea Everton baada ya kupita miaka 13, anatarajiwa kuwa kwenye kikosi cha
timu hiyo ambacho kitatua Tanzania kwa ajili ya mechi moja ya kirafiki dhidi ya
Gor Mahia ya Kenya.
Akizungumza
na luninga ya klabu hiyo, Rooney amesema anaisubiri kwa hamu ziara hiyo ya
kwenda Tanzania kani anadhani itakuwa safari nzuri itakayomuwezesha kufahamiana
vyema na wenzake.
Rooney
aliendelea kuwa ziara kama hizo huwa nzuri kwani ni vizuri kukaa hotelini na
wachezaji, kujumuika nao na kuwafahamu zaidi.
Rooney
amesema hajawahi kufika Tanzania hivyo ana hamu kubwa ya kutua katika taifa
hilo la Afrika Mashariki.
No comments:
Post a Comment