Kocha
mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Salum Shaban Mayanga ametangaza
kikosi kitakachoikabili timu ya taifa ya Rwanda katika mchezo wa kuwania kufuzu
fainali za mataifa za mataifa bingwa ya Afrika CHAN utakaochezwa jijini Mwanza
mwishoni mwa juma hili.
Mayanga
amewaondoa baadhi ya wachezaji aliokwenda nao Afrika kusini kwenye michuano ya
ukanda wa Afrika kusini, ambao wanaokosa sifa ya kushiriki michuano ya
CHAN ambayo inatoa fursa kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani pekee.
Mayanga
amesema kikosi chake kitaweka kambi kwa siku kadhaa jijini Mwanza kabla ya
kucheza na Rwanda, na anaamini muda uliosalia unatosha kukiandaa kikosi chake.
No comments:
Post a Comment