James
Rodriguez ameamua kwamba Manchester
United ndio klabu pekee ambayo angependa kuhamia majira haya ya kiangazi, kwa
mujibu wa taarifa kutoka Diario Gol.
Nyota huyo
wa kimataifa wa Colombia
ambaye msimu uliopita alicheza jumla ya mechi 33 ,
hakuweza kuingia kwenye kikosi cha jumla cha Zinedine Zidane katika mechi ya
fainali ya UEFA.
Amemuambia
Rais wa klabu hiyo , Florentino Perez, kwamba atabaki Real Madrid kama
hatoruhusiwa kuongea na Manchester United, na hiyo itazidi kumletea Zidane
maumivu ya kichwa.
No comments:
Post a Comment