Wakati
kesho Jumatano Julai 5, 2017 timu yetu ya Tanzania ya mpira wa miguu -
(Picha na soka360tz)
Taifa
Stars ikicheza na Zambia katika Nusu Fainali ya kuwania Kombe la Castle COSAFA,
Kocha Mkuu Salum Shaban Mayanga amemuongeza kwenye kikosi Mshambuliaji John
Raphael Bocco.
Bocco kwa sasa yuko Afrika Kusini pamoja na
timu hiyo akichukua nafasi ya Mshambuliaji Mbaraka Yussuf Abeid aliyejepata
majeruhi kwenye michuano hiyo iliyoanza Juni 25, mwaka huu ambako Tanzania
ilikuwa Kundi ‘A’ pamoja na timu za Malawi, Mauritius na Angola.
Tanzania iliibuka kinara katika kundi hilo na
kucheza Robo Fainali ambako ilicheza na Afrika Kusini na kuitoa katika hatua
hiyo hivyo kwa mujibu wa ratiba, kesho Jumatano Julai 5, mwaka itashindana na
Zambia.
Kocha Salum Mayanga amefafanua kuwa mbali ya
Bocco kujaza nafasi hiyo, amemwongeza kwenye kikosi ili kuongeza nguvu ya
kupambana na Rwanda katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya
Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani - CHAN.
Mchezo dhidi ya Rwanda utafanyika Julai 15,
mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza. Mchezo wa marudiano
utafanyika baadaye mwezi huu na mshindi wa jumla atacheza na Uganda ambako
mshindi wa jumla atakuwa amefuzu kwa fainali hizo zitakazofanyika Kenya, mwaka
2018.
No comments:
Post a Comment