MENEJA wa
Manchester United, Jose Mourinho amedaiwa kutofurahishwa na taratibu za klabu
hiyo katika usajili wa kipindi hiki cha kiangazi.
Baada ya
United kutwaa taji la michuano ya Europa League Mei 24 mwaka huu, Mourinho
amesema alimpa makamu mwenyekiti Ed Woodward orodha na wachezaji anawahitaji
katika usajili.
Taarifa za
ndani zinadai kuwa orodha hiyo ilikuwa na mahitaji machache ya wachezaji watatu
au wanne pekee.
Kuna
uwezekano kukawa na maendeleo mengine wiki hii lakini mpaka sasa ni mchezaji
mmoja mpya aliyesajili ambaye ni beki wa Benfica, Victor Lindelof aliyetua Old
Trafford kwa kitita cha paundi milioni 31.
Inaaminika
kuwa Mourinho anataka angalau mshambuliaji mmoja ili kuziba nafasi ya Zlatan
Ibrahimovic pamoja na mchezaji wa nafasi ya kiungo wa ulinzi.
No comments:
Post a Comment