TIMU ya
Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo inashuka katika dimba la Moruleng Kucheza na
Zambia katika mchezo wa nusu fainal ya kombe la COSAFA mchezo utakaochezwa saa
kumi na mbili kamili kwa saa za afrika mashariki.
Taifa stars
imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kumwondosha mwenyeji Afrika ya Kusini
kwenye hatua ya Robo fainali kwa ushindi wa bao 1 lililofungwa na Eias Maguli
katika kipindi cha kwanza.
Taifa stars
ambayo imecheza michezo minne bila kufungwa ambapo imeshinda michezo miwili na
kutoka sare michezo miwili katika mashindano
ya COSAFA, leo inashuka kuwakabili
Zambia katika mchezo wa nusu fainali.
No comments:
Post a Comment