Saturday, 1 July 2017

MASHABIKI WA SIMBA WAOMBWA KUWA WATULIVU.



Wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba wameombwa kuendelea  kuwa kitu kimoja katika kipindi hiki ambacho viongozi wao wa ngazi za juu wanakabiliwa na tuhuma za utatatishaji wa fedha.


Rai hiyo kwa wanachama na mashabiki wa klabu ya Simba imetolewa na mjumbe wa kamati ya utendaji ya klabu hiyo Said Tully
ambapo amesema hawana budi kukubaliana na hali halizi inayowakabili viongozi wao.

Amesema pamoja na kutokuwepo kwa rais wao Evance Aveva na makamu wake Geoffrey Nyange Kaburu bado shughuli za klabu ya Simba zitaendelea kufanyika.

Hata hivyo Said Tully amesema suala la nani atakaimu nafasi za rais na makamu wa rais wa klabu ya SImba bado litakua sehemu ya kikao cha kamati ya utendajhi kitakachoketi kesho jijini Dar es salaam, hivyo ameendelea kuwasisitiza mashabiki na wanachama kuwa watulivu.

No comments:

Post a Comment