Kamati
ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, iliyokutana leo Jumamosi
Julai 01, 2017 kwenye ofisi za TFF, Dar es Salaam imempitisha Wallace Karia
kuwa Kaimu Rais wa shirikisho.
Kadhalika,
Kamati hiyo ya Utendaji ya TFF, imempitisha Mkurugenzi
wa Ufundi wa TFF, Salum
Madadi kuwa Kaimu Katibu Mkuu wa TFF.
Viongozi
hao watakaimu nafasi hizo tajwa hadi hapo mahakama itakavyoamua kuhusu kesi
zinazowakabili kwa sasa Rais wa TFF, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu, Mwesigwa
Selestine.
Kamati
ya Utendaji ya TFF, imekutana kwa dharura kwa mujibu wa Ibara ya 35 (1)
inayosomwa pamoja na Ibara ya 35 (6) na kufanya uamuzi huo.
No comments:
Post a Comment