Kamati
ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyokutana Julai
8, mwaka huu pamoja na mambo mengine pia ilijadili mchakato wa chaguzi za Mkoa
wa Rukwa (RUREFA) na timu ya Lipuli inayoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom.
Kuhusu
mchakato wa uchaguzi Mkoa wa Rukwa (RUREFA), Kamati ya Uchaguzi inayoongozwa na
Mwenyekiti Msomi Wakili Revocatus Kuuli, imeagiza zoezi hilo liendelee na
inamtuma Mjumbe wake siku ya usaili, Msomi Wakili Thadeus Karua kwa ajili ya
kushuhudia.
“Na
pia Kamati ya Uchaguzi itawatuma wajumbe siku ya uchaguzi tarehe 5 Agosti,
2017,” imesema kamati hiyo ilipoagiza kuhusu kuendelea kwa uchaguzi huo.
Kuhusu
uchaguzi wa Lipuli, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Msomi Wakili Kuuli,
imemwagiza Katibu Mkuu wa klabu hiyo, kuendelea na maandalizi ya uchaguzi kama
ilivyoelekezwa na kamati kwamba ufanyike Agosti 5, mwaka huu.
“Na
Kamati inamtuma mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi Msomi Wakili Mohamed Ally
Mchungahela kwa ajili ya uangalizi siku ya uchaguzi,” imesema sehemu ya taarifa
ya kamati kwa uongozi wa Lipuli.
Kamati
imesisitiza, “Na wanachama waendelee kulipia ada za uanachama kwa kuwa
watakaoruhusiwa kupiga kura ni wanachama hai tu.”
No comments:
Post a Comment