
BEKI wa kati ya klabu ya
Barcelona Marc Bartra amesema ameshangazwa kwa kukosekana kwa Luis
Suarez katika orodha ya kugombea tuzo za Ballon d’Or. Nyota huyo wa
kimataifa wa Uruguay alifunga mabao 31 katika mechi 33 akiwa na
Liverpool msimu uliopita huku 12 kati hayo akiwa amefunga mwaka huu na
kutoa pasi za kusaidia 11. Lakini pamoja na mafanikio hayo, Suarez
anaonekana bado kuandamwa na mzimu wa kumng’ata Giorgio Chiellini wa
Italia katika Kombe la Dunia nchini Brazil na kumfanya kufungiwa miezi
minne adhabu ambayo aliimaliza wiki iliyopita. Bartra anaamini
mshambuliaji huyo ambaye alitengeneza bao la Barcelona lililofungwa na
Neymar katika mchezo wa El Clasico dhidi ya Madrid, alitakiwa kuwepo
katika orodha hiyo. Akihojiwa beki huyo mwenye umri wa miaka 23 amesema
maeshangazwa kwa Suarez kuachwa kwani anadhani alikuwa na mwaka wenye
mafanikio.
No comments:
Post a Comment