Kamanda wa kanda maalumu ya DSM Suleiman Kova akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema mapromota hao wanashikiliwa kwa kukiuka mkataba na kutoweka huku wakimwacha bondia huyo mmarekani kushindwa kuondoka nchini akidai malipo yake.
Pambano hilo la WBF licha ya Cheka kuibuka na ushindi lilitawaliwa na dosari kadhaa zilizochangiwa na mapromota hao zikiwemo baadhi ya mabondia kugoma kupanda ulingoni wakitaka kwanza walipwe haki zao.
Wakati huo huo jeshi la polisi linawashikilia watu wanne baada ya kukutwa na Copyuta nne zilizokuwa zikitumika kudurufu kazi za wasanii mbali mbali wakiwemo wa muziki pamoja na filamu.
No comments:
Post a Comment