Meneja wa Chelsea ,Jose Mourinho anategemea kupunguza machungu yake ya kumkosa Wayne Rooney kwa kumsajili Samuel Eto’o, 32, wa Anzhi Makhachkala na Christian Atsu, 21 wa FC Porto.
Mshambuliaji mwenye asili ya Cameroon, Eto’o atatambulishwa kama mchezaji wa Chelsea siku ya Alhamisi.
Sunderland wamekutana na ushindani dhidi ya Rennes kumsajili Beki wa Senegal, Cheikh M’Bengue, 25.
West Ham wanaweza kumkosa Oscar Cardozo, 30, baada ya Barcelona kuonyesha nia ya kumsajili Mshambuliaji huyo wa Benfica.
Meneja wa Tottenham, Andre Villas-Boas anataka kumsajili Mshambuliaji wa Manchester United, Javier Hernandez, 25, lakini wanatakiwa kulipa kiasi cha £15m kumpata Mshambuliaji huyo mwenye asili ya Mexico
Arsenal wako tayari kutoa dau kwa Kiungo wa St Etienne, Josuha Guilavogui, 22, kama watamkosa Yohan Cabaye, 27 ,wa
on Newcastle.
UDAKU WA KIDUNIA
Paris St-Germain wameonyesha nia ya kutaka kumsajili golikipa wa Real Madrid Iker Casillas ,32, ambaye amekuwa akiwekwa benchi tangu ujio wa Carlo Ancelotti ndani ya Bernabeu.Mesut Ozil, 24, ameondoa fununu zote zilizosikika ya kwamba anataka kuhama kwa kusema angependa kuendelea kubaki Real Madrid.Ilisemekana Mjerumani huyo anataka kuondoka sababu ya ujio wa Gareth Bale, 24.
Lazio wako katika majaribio ya kutaka kumsajili Mshambuliaji Mturuki Burak Yilmaz, 28, kutoka Galatasaray.
Klabu kutoka Bundesliga ya Schalke wanakaribia kumsajili Kiungo, Dennis Aogo, 26, kutoka Hamburger SV katika mkataba wa mkopo kwa mwaka mmoja wakiwa na matumaini ya kumsajili baadae.
UDAKU MWINGINE
Mshambuliaji wa Ivory Coast, Gervinho, 26, amekiri ya kwamba amefurahi kuihama Arsenal na amedhamiria kupandisha kiwango chake akiwa klabu yake mpya ya Roma.
Mashabiki wa Borussia Dortmund wako kwenye kampeni ya kushinikiza Shinji Kagawa, 24, aondoke Manchester United na kurudi Ujerumani.
No comments:
Post a Comment