Kamati
ya Uchaguzi ya Chama cha Wataalamu wa Tiba za Michezo (TASMA), kimetangaza
majina ya waliochukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa
chama hicho unaotarajiwa kufanyika Agosti 5, mwaka huu.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya chama hicho, Leslie Liunda
wanaowania uenyekiti ni Joakim Mshanga, Usubene Kisongo na Biyondo Mgome
ilihali kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti, amejitokeza Magreth Mtaki pekee.
Wale
wanaotaka ukatibu mkuu wa chama hicho ni Suphian Juma na Nassoro Matuzya
waliojitokeza huku nafasi ya ukatibu msaidizi inawaniwa na Alfred Mchinamnamba.
Nafasi
Mweka Hazina inawaniwa Alex Gongwa huku Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF inawaniwa
Richard Yomba na Cosmas Kapinga ilihali Ujumbe wa Kamati ya Utendaji wamo
Paschal Itonge na Mwanandi Mwankemwa.
Kwa
mujibu wa ratiba ya mchakato wa uchaguzi huo kuanza leo na kesho (Julai 18,
2017 na Julai 19, mwaka huu) watapokea pingamizi katika ofisi za Omlipiki
Maalumu (Special Olympic) zilizopo jirani na Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kipindi
cha usaili kimepangwa kuanza Julai 20, 2017 hivyo wagombea wote wanatakiwa
kufika mbele ya kamati ili kusailiwa.
“Mgombea
ambaye atashindwa kuhudhuria atakuwa amejiondoa kwenye kinyang’anyiro cha
uchaguzi utafanyika Agosti 5, mwaka huu katika Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni,
Dar es Salaam,” amesema Liunda.
No comments:
Post a Comment