Benchi
la ufundi la klabu ya Simba,chini ya kocha wake mkuu Joseph Omog limefanya
marekebisho kwenye eneo la unahodha wa timu.
Katika
marekebisho hayo yaliyoridhiwa na uongozi wa klabu,beki wa kimataifa Mzimbabwe
Method Mwanjale ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa timu ya Simba,akichukua nafasi
ya Jonas Mkude atakaendelea kuwa mchezaji mwandamizi kwenye kikosi
hicho,ambacho kwa sasa kipo nchini Afrika kusini kujiandaa na msimu mpya
unaotarajiwa kuanza mwezi ujao.
Kwenye
mabadiliko hayo ya kawaida, benchi la ufundi pia limewateua Mchezaji bora wa
ligi kuu ya Tanzania na klabu ya Simba kwa msimu huu,Mohammed
Hussein(Tshabalala)na John Raphael Boko kuwa manahodha wasaidizi wa timu
hiyo.
Klabu
inamshukuru sana Nahodha wake kwenye msimu uliopita na mchezaji wake
mwandamizi,Jonas Mkude kwa kazi nzuri alioifanya muda wote alipokuwa Nahodha wa
Timu.
Kwa
sasa kikosi chetu kinaendelea na mazoezi na kila kitu kinakwenda vema huko
kambini Eden Vale Johannesburg nchini Afrika kusini.
No comments:
Post a Comment