Michuano hiyo ilianza kutimua vumbi jana kwa mchezo mmoja kuchezwa katika uwanja wa Karume uliopo mjini Musoma, ambapo Vill Squad ya jijini Dar es salaam iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 3- 1 dhidi ya timu ya JKT Rwamkoma ya mkoani Kagera.
Katika uwanja wa CCM Kirumba, Pamba FC ya jijini humo watakua wenyeji wa timu ya wachimba dhahabu kutoka mkoani Shinyanga, Bulyanhulu FC mchezo utakaoza saa 10:30 jioni.
Jumla ya timu 64 zinashiriki michuano hiyo kutoka Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kuwania kutwaa ubingwa, ambapo Bingwa wa michuano AzamHD Federation Cup atapata nafasi ya kuwakilisha nchi kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment