KATIKA habari za tetesi za usajili
zilizojitokeza hii leo ni pamoja na klabu ya AS Roma wakibakia na matumaini ya
kumsajili Petr Cech kutoka Chelsea
pamoja na Jose Mourinho kusisitiza kuwa
golikipa huyo hatauzwa katika kipindi hiki cha Januari.
Kwa upande wa Liverpool wao
wamekubali kutoa kitita cha paundi milioni 10 kwa ajili ya kkumsajili nyota wa
Bayern Munich Xherdan Shaqiri huku wakiwa na matumaini ya kuzipiga bao Arsenal
na Manchester United ambao nao wamekuwa wakimuwinda nyota huyo wa kimataifa wa
Uswis.
Klabu ya Arsenal nayo inaripotiwa
kutenga kitita cha paundi milioni 64 kwa ajili ya kumuwania Isco kutoka klabu
ya Real Madrid. Arsenal wametenga dau hilo hilo litakaloweza kuvunja rekodi ili
kuwazidi kete Chelsea, Liverpool na Manchester City ambao nao wamekuwa
wakimtolea macho nyota huyo wa kimataifa wa Hispania.
Tukibaki hapohapo Arsenal
wanaripotiwa kutupiwa ofa yao ya kumsajili chipukizi wa klabu ya Legia Warsaw
Krystian Bielik. Mazungumzo baina ya vilabu hivyo bado yanaendelea huku
ikiripotiwa kuwa Legia wanataka kitita cha paundi milioni 2.3 kwa ajili ya
kinda huyo.
Nayo klabu ya Newcastle United imeihabalisha
klabu ya Paris Saint-Germain-PSG kuwa hawatamuuza Moussa Sissoko kwa dau la
chini ya paundi milioni 25.
Newcastle wamepania kuendelea kubaki na kiungo
huyo hadi mwisho wa msimu huu. Kwa upande mwingine klabu ya West Bromwich
Albion imekubali kuwauzia Tottenham Hotspurs mshambuliaji wao Saido Berahino
lakini kwa makubaliano ya Spurs nao kuwatoa Aaron Lennon na Andros Townsend.
Inadaiwa kuwa West Brom wako tayari
kumuuza mshambuliaji huyo lakini na wao wanahitaji kuimarisha kikosi chao.
No comments:
Post a Comment