Barcelona wanamtaka Ander Herera na Riyad Mahrez, kama
watashindwa kumsajili Marco Verratti (Sport.es).
Arsenal wamejitoa katika mbio za kumwania nyota wa Monaco
Kylian Mbappe, 18, na sasa wataelekeza nguvu zao kumpata Alexandre Lacazette na
Thomas Lemar (Mail Online).
Antonio Conte hajafurahishwa na hatua ya Chelsea kumfuatilia Romelu Lukaku badala ya Andrea Belotti. Conte ameghadhibishwa kwa sababu wachezaji hao wawili bei yao ni moja, takriban pauni milioni 85, lakini mkurugenzi wa ufundi wa Chelsea Michael Emenalo ameamua kumfuatilia Lukaku badala ya Belotti (Daily Star).
Guangzhou Evergrande hawana mpango wowote wa kumuuza Paulinho kwenda Barcelona (Nanfang Daily).
Alvaro Morata amewaambia marafiki wake kuwa ameamua kujiunga
na Manchester United na kuwa mkataba tayari "umekamilika" (Daily
Express).
No comments:
Post a Comment