Leon Goretzka alifunga mara mbili katika mtanange huo katika dakika ya 6 na
8.
Magoli mengine ya Ujerumani yaliwekwa kimiani na Timo Werner dakika ya 59 na
Amin Younes dakika ya 90.
Goli la kufutia machozi kwa upande wa Mexico lilipachikwa na Marco Fabian
dakika ya 89.
Mexico walipata nafasi nyingi lakini hawakuweza kuzitumia vyema huku
Ujerumani ikionekana kukomaa vilivyo katika safu ya ulinzi.
Fainali ya kombe la mabara itapigwa jumapili ya Julai 2
mbili kati ya Ujerumani na Chile mjini St Petersburg, huku mchezo wa awali
ukizikutanisha Ureno na Mexico kutafuta mshindi wa tatu.
No comments:
Post a Comment