Mchezaji
nyota wa duniani Lionel Messi amefunga
pingu za maisha na mpenzi wake wa tangu utotoni katika mji wake wa kuzaliwa
nchini Argentina.
Mchezaji
huyo wa Barcelona amerejea katika jiji la Rosario na kufunga ndoa na
Antonella Roccuzzo,
ambaye walikutana kabla yake kuhamia Uhispania akiwa na miaka 13.
Wachezaji
wenzake Messi, wakiwemo Luis Suárez na Neymar, walikuwa miongoni mwa wageni 260
waliohudhuria sherehe hiyo, kwa mujibu wa tovuti ya BBC SWAHILI.
Katika
tukio hilo Maafisa wa polisi wametumwa katika mji huo kudumisha usalama katika
hoteli wanamokaa, na kampuni ya kibinafsi ya usalama itadumisha ulinzi ndani
kuzuia watu wasioalikwa kuingia.
No comments:
Post a Comment