MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich,
Thomas Muller amekuwa mchezaji mdogo zaidi kupata ushindi wa mechi 50 za Ligi
ya Mabingwa Ulaya kufuatia timu hiyo kuichapa Olympiakos jana.
Muller akiwa na umri wa miaka 26
amefikia rekodi hiyo akiwa mdogo kwa mwaka mmoja kuliko Lionel Messi na karibu
mdogo kwa miaka miwili kuliko Cristiano Ronaldo.
Nyota huyo wa kimataifa wa Ujerumani
ambaye alicheza michuano hiyo kwa mara ya kwanza Macho mwaka 2009, alifunga bao
moja katika ushindi wa mabao 4-0 waliopata dhidi ya Olympiakos.
Akihojiwa Muller ambaye amefikia rekodi kwa
kucheza mechi 75, amesema amefikia rekodi hiyo kwasababu anacheza katika klabu
nzuri.
No comments:
Post a Comment