NGULI wa zamani wa Liverpool, Steven
Gerrard amethibitisha kurejea katika klabu hiyo wiki ijayo lakini kwa ajili ya
kufanya mazoezi pekee.
Kiungo huyo mkongwe wa klabu ya Los
Angeles Galaxy mwenye umri wa
miaka 35 amekuwa akihusishwa na tetesi za kurejea
kufuatia msimu wa Ligi Kuu ya Marekani-MLS kusimama.
Lakini nyota huyo wa zamani wa
Uingereza alikanusha tetesi hizo na kudai kuwa atakwenda Anfield kwa ajili ya
kufanya mazoezi chini ya meneja wa sasa Jurgen Klopp.
Akihojiwa Gerrard amesema ana hamu
kubwa ya kujifunza kutoka kwa Mjerumani huyo wakati atapokwenda kufanya nao
mazoezi wiki ijayo.
Gerrard ameitumikia Liverpool kwa
miaka 17 kabla ya kuamua kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment