TANZANIA
imetolewa katika mbio za kugombania tiketi ya kufuzu kucheza fainali za
Kombe la Dunia za mwaka 2018 zitakazofanyika nchini Urusi, baada ya
kufungwa mabao 7-0 usiku huu na wenyeji Algeria katika mechi iliyochezwa
Uwanja wa Mustapha Tchaker mjini Blida.
Matokeo
hayo, yanaifanya Taifa Stars itolewe kwa jumla ya mabao 9-2, baada ya
awali kulazimishwa sare ya 2-2 na Mbweha hao wa Jangwani katika mechi ya
kwanza iliyochezwa Jumamosi mjini Dar es Salaam.
kwa mantiki hiyo stars inarudi nyumbani kujipanga upya kwa michuano mingine,
No comments:
Post a Comment