Nahodha
na mshambuliaji wa timu ya taifa ya England, Wayne Rooney, hiii leo
hatoanzishwa kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo, katika mchezo wa kimataifa
wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Hispania.
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson amethibitisha
kumuweka pembeni mshambuliaji huyo, kwa lengo la kumpumzisha na kutoa nafasi
kwa wachezaji wengine.
Hodgson,
amesema tayari ameshazungumza na Rooney juu ya jambo hilo, na wamekubaliana kwa
dhati hivyo anatarajia kumtumia mshambuliaji tegemeo wa klabu ya Leicester City, Jamie
Vardy, ambaye amemuita kikosini kutokana na umahiri mkubwa anaoendelea
kuuonyesha katika ligi ya nchini England.
Amesema
maamuzi hayo katu hayawezi kuathiri mfumo atakaoutumia kikosini mwake, kutokana
na kuamini kwamba Jamie Vardy, anatosha kuziba pengo la Wayne Rooney ambaye pia
ni nahodha wa Man Utd.
Hata
hivyo amewahakikishia mashabiki wa soka nchini England na kwingineko duniani
kote, kwa kusisitiza kumtumia Rooney katika kikosi chake cha kwanza ambacho
kitapambana na timu ya taifa ya Ufaransa kati kati ya juma lijalo.
No comments:
Post a Comment