Wednesday, 11 November 2015

MBWANA SAMATTA NA THOMAS ULIMWENGU WAWASHUKURU WATANZANIA KWA KUWAOMBEA.



Baada ya kurejea nchini wakitoke nchini Congo DRC wachezaji wa Tanzania MBWANA SAMATTA na THOMAS ULIMWENGU Mkuuu wa mkoa wa Dar es Salaam SAID MECKY SADICK ameawapongeza wachezaji hao baada ya kufanya vizuri katika klabu yao ya TP Mazembe ya huko Congo.


Kwa upande wake mchezji MBWANA SAMATTA amewashukuru watanzania waliomuunga mkono katika kipindi alichokuwa jijini Lumbumbashi huku  akiweka mkazo zaidi kwa sasa katika mchezo wao wa jumamosi dhidi ya timu ya Algeria pamoja na klabu yake kutwa kombe hilo.


Naye THOMAS ULIMWENGU amesema kwa sasa wao wanachaangalia ni kusonga mbele na kuweka nguvu zaidi katika mchezo wao huo pamoja na yaote yaliyotokea jumapili iliyopita walipocheza dhidi ya klabu ya USM Algers.


Klabu ya TP mazembe jumapili iliyopita ilitwaa kikombe cha klabu bingwa Afrika baad ya kuwatandika klabu ya Algers katika fainali iliyochezwa jijini Lubumbashi kwa mabao 2-0  huku MBWANA SAMATTA akifunga bao moja katika mchezo huo.

No comments:

Post a Comment