Thursday, 12 November 2015

MATOLA ASEPA SIMBA "KWANII NA IMEKUWAJE"



KOCHA Msaidizi wa Simba SC, Suleiman Abdallah Matola amejiuzulu nafasi hiyo kutokana na kile alichodai kutolelewana na Kocha Mkuu, Muingereza, Dylan Kerr.

Akizungumza na OKAMA BLOG mchana wa leo msemaji mkuu wa klabu ya soka ya samba HAJI MANARA amesema matola ameongea na rais wa klabu ya soka ya simba na kumwambia hataki kuendelea kuwepo kwenye banchi la ufundi ya simba kutokana na ugomvi wake na na kocha mkuu wa klabu hiyo kerr.


Historia ya Matola ndani ya Simba SC inaanzia mwaka 2000 alipojiunga nayo kama mchezaji akitokea Kagera Stars (sasa Kagera Sugar) na aliichezea timu hiyo hadi mwaka 2005 alipohamia Super Sport United ya Afrika Kusini.

Matola alirejea Simba SC mwaka 2007 na kucheza kwa msimu mmoja kabla ya kustaafu moja kwa moja.
 
Kuanzia mwaka 2010 amekuwa kocha wa timu za vijana za Simba SC ambako baada ya kufanya vizuri akapandishwa kuwa Kocha Msaidizi, akianza kufanya kazi na Mcroatia Zdravko Logarusic, baadaye Mzambia, Patrick Phiri, Mserbia, Goran Koponovic na huyu wa sasa Kerr.

Haijawahi kutokea Matola akatofautiana na kocha yeyote kati aliyofanya nao kazi awali – na Muingereza huyu anakuwa wa kwanza kutofautiana na Nahodha wa zamani wa Simba SC.

No comments:

Post a Comment