WINGA wa Real Madrid, Gareth Bale amesema yuko tayari kwa
mapambano wakati kikosi chao kikijiandaa kwa ajili ya mchezo wa Clasico dhidi
ya mahasimu wao Barcelona kesho.
Nyota huyo wa kimataifa wa Wales, mwenye umri wa miaka 26,
alikuwa amepata majeruhi ya nyonga Octoba mwaka huu na kukosa michezo minne
kabla ya katika mchezo waliofungwa na Sevilla Novemba 8. Akihojiwa Bale amesema
amekuwa majeruhi kwa wiki sita hivyo hajapata muda wa kutosha kucheza msimu huu
lakini anajisikia imara na fiti kwa ajili ya mchezo wa kesho.
Madrid watakwenda katika mchezo huo wakiwa alama tatu nyuma
ya Barcelona ambao wanaweza kuwa na mshambuliaji wao nyota Lionel Messi baada
ya kupona majeruhi ya goti waliyopata Septemba mwaka huu.
Messi ambaye ndio mfungaji kinara wa Clasico akiw na mabao
21, amerejea mazoezini na anaweza kurejea katika safu ya ushambuliaji ya
Barcelona sambamba na nyota wenzake Luis Suarez na Neymar.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ulinzi wa hali ya juu
kufuatia tukio ya mashabulio ya kigaidi ya Paris, ambapo karibu walinzi wa
kujitegemea 1,500 wanatarajiwa kufanya kazi wakati wa mchezo huo wakishirikiana
na polisi wapatao 1,000.
WINGA wa Real Madrid,
Gareth Bale amesema yuko tayari kwa mapambano wakati kikosi chao
kikijiandaa kwa ajili ya mchezo wa Clasico dhidi ya mahasimu wao
Barcelona kesho. Nyota huyo wa kimataifa wa Wales, mwenye umri wa miaka
26, alikuwa amepata majeruhi ya nyonga Octoba mwaka huu na kukosa
michezo minne kabla ya katika mchezo waliofungwa na Sevilla Novemba 8.
Akihojiwa Bale amesema amekuwa majeruhi kwa wiki sita hivyo hajapata
muda wa kutosha kucheza msimu huu lakini anajisikia imara na fiti kwa
ajili ya mchezo wa kesho. Madrid watakwenda katika mchezo huo wakiwa
alama tatu nyuma ya Barcelona ambao wanaweza kuwa na mshambuliaji wao
nyota Lionel Messi baada ya kupona majeruhi ya goti waliyopata Septemba
mwaka huu. Messi ambaye ndio mfungaji kinara wa Clasico akiw na mabao
21, amerejea mazoezini na anaweza kurejea katika safu ya ushambuliaji ya
Barcelona sambamba na nyota wenzake Luis Suarez na Neymar. Mchezo huo
unatarajiwa kuwa na ulinzi wa hali ya juu kufuatia tukio ya mashabulio
ya kigaidi ya Paris, ambapo karibu walinzi wa kujitegemea 1,500
wanatarajiwa kufanya kazi wakati wa mchezo huo wakishirikiana na polisi
wapatao 1,000.
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
Copy the BEST Traders and Make Money : http://bit.ly/fxzulu
No comments:
Post a Comment