"Thanks to
everyone at WWE for a great night, the kids loved it. Hope you're ok Wade
Barrett! Haha………"
Mshambuliaji
wa Manchester United Wayne Rooney,Ryan Giggs,Darren Fletcher,Bingwa wa zamani
wa WWE John Bradfield Layfield na mtoto wa Wayne Rooney,Kai jana walihudhuria
mchezo wa Mieleka,WWE,jijini Manchester.
Katika
mchezo huo,mfalme wa WWE,Wade Barrett alianza kumchokonoa Wayne Rooney kwa
kusema "katika huu ulingo kuna wanaume wawili ambao wanahadhi ya
ubingwa,yeah ni kweli,lakini si Wayne Rooney na Manchester United"
Barrett
akawa anamtaka Rooney apande ulingoni na Rooney akasema shuka huku chini,
Barrett akaendelea kumchokonoa Rooney akisema " Ninamchukia huyo mwanao
(Kai),amekaa hapo akishuhudia baba yake akifeli hahahah ", Rooney
akakasirika
Rooney
akaamua kusimama na Barrett akamfata pale, ndipo Rooney akampiga kibao
kimoja,Barrett akaanguka chini na mashabiki wote uwanjani wakashangilia .
Baada ya
pambano hilo kumalizika Barrett alitwit " Kesho ninaenda Old Trafford
nataka nikakutane na Rooney huko"
WWE ambao
waliandaa tukio hilo kabla walimshukuru Wayne Rooney kwa kukubali kushiriki
pambano hilo na kuwafurahisha mashabiki.
Barrett
ambaye ni mshabiki wa Klabu ya Preston North End alishawahi kumkosoa Wayne
Rooney kwa kujiangusha na kupata Penati na kusababisha timu yake kutolewa na
Man United katika kombe la FA mwezi Februari mwaka jana
No comments:
Post a Comment